Page 1 of 1

Kilimo na Ufugaji, Jakaya Kikwete, Salumu Sumry na Mizengo Pinda Waonyesha Njia

Posted: Fri Oct 27, 2017 11:20 am
by RealityKing
Biashara ya kilimo na ufugaji nchini Tanzania huenda miaka michache ijayo ikawa na tija katika kuajiri na kuchangia pato la Taifa kuliko ambavyo imekuwa kwa miaka mingi. Sekta za kilimo na ufugaji nchini Tanzania hazijapewa kipaumbele na serikali kwa kiwango kinachostahili hasa ukizingatia ni sekta zinazoajiri watanzania zaidi ya asilimia 80.

Hata hivyo mambo huenda yakabadilika miaka kadhaa ijayo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na watu maarufu kuanza kuonyesha njia kwa kufanya kilimo cha kisasa. Mfano wa watu hao ni aliyekuwa Rais wa awamu ya nne wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye hivi sasa ni mkulima na mfugaji wa ng'ombe.



Mwingine ni Salumu Sumry, aliyekuwa mmiliki wa mabasi ya Sumry ambaye ameachana na biashara ya usafiri wa mabasi na kujiingiza katika biashara ya kilimo, hasa cha mahindi. Salumu aliachana na biashara ya mabasi, wakati huo akiwa anamiliki mabasi 81.



Vilevile kuna habari za uhakika kuwa Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne, ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda, naye ni mkulima na mfugaji hivi sasa.


Re: Kilimo na Ufugaji, Jakaya Kikwete, Salumu Sumry na Mizengo Pinda Waonyesha Njia

Posted: Tue Oct 31, 2017 9:44 am
by Joseph Bundala
Ni jambo jema sana hili, ninachoona ni kuwa watu wenye kipato cha wastani ni changamoto kwao kufanya kilimo kama hiki. Mtaji na nia inahitajika. Halafu kile kilimo cha kupiga simu shamba huku ukiwa mjini ni patapotea pia.

Re: Kilimo na Ufugaji, Jakaya Kikwete, Salumu Sumry na Mizengo Pinda Waonyesha Njia

Posted: Wed Nov 01, 2017 11:13 am
by Eli
@Simulink

Kilimo unatakiwa ujipeleke mwenyewe na usimamie kwelikweli. Bado naamini kuwa serikali yetu inatakiwa kutoa kipaumbele cha kipekee katika sekta ya kilimo kwa sababu ndiyo inayoajiri asilimia kubwa ya watanzania.

Re: Kilimo na Ufugaji, Jakaya Kikwete, Salumu Sumry na Mizengo Pinda Waonyesha Njia

Posted: Wed Sep 25, 2019 12:18 am
by Eli