Page 1 of 1

Dunia Uwanja wa Fujo

Posted: Wed Nov 02, 2016 1:33 pm
by Eli
"Dunia uwanja wa fujo ni riwaya iliyoandikwa na mwandishi Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975, ni riwaya ambayo inasawili maisha ya wanadamu hususani waishio Afrika Mashariki hasahasa katika nchi ya Tanzania.

“Dunia uwanja wa fujo” inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawa sawa na fujo kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadae kutoweka. Mwandishi E. Kezilahabi anaelezea katika jamii kila mtu anakuja duniani kufanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama vile mauaji , ukabila, umalaya, uchawi, ubakaji ulevi wa kupindukia nk. hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka, mfano mhusika Tumaini katika Riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya, mauaji na mengine mengi na baadae kutoweka." Endelea kusoma

Wapi napata kitabu cha Willy Gamba kijulikanacho kama "Njama"? Nilisimuliwa kuhusu hicho kitabu, sijawahi kukisoma, nadhani ni kizuri.