PIGIA KURA MAJINA YA SAYARI-NJE NA NYOTA ZA TANZANIA (Vote for Tanzania ExoWorld Names) - Mwisho wa Kupiga Kura 14/11/19

Post general but valuable information and news and information: tech and/or education-related news and announcements. Posts under this forum must strictly adhere to the Forum Rules. If you are not sure about what to post, please ask for help from forums administration. Any violation will not be tolerated!
Locked

Chagua siyo zaidi ya jozi tatu unazopenda kati ya hizi zifuatazo, halafu bonyeza Submit vote

Sayari-nje: TANZANITE; Nyota-mama: MPINGO (Angalia sababu)
70
19%
Sayari-nje: CHUNGWA; Nyota-mama: BOGA (Angalia sababu)
58
15%
Sayari-nje: UHURU; Nyota-mama: KIBO (Angalia sababu)
80
21%
Sayari-nje: NEUPLADIS; Nyota-mama: LUNYADU (Angalia sababu)
5
1%
Sayari-nje: ISIMILA; Nyota-mama: EIBOR-NiLIIL (Angalia sababu)
18
5%
Sayari-nje: HOMO; Nyota-mama: TSETSEI (Angalia sababu)
45
12%
Sayari-nje: CHANDISI; Nyota-mama: GIRAG (Angalia sababu)
8
2%
Sayari-nje: IWAHA; Nyota-mama: DEKA (Angalia sababu)
7
2%
Sayari-nje: TANZANITE; Nyota-mama: KILI (Angalia sababu)
63
17%
Sayari-nje: MBOZI; Nyota-mama: OLDONYO-LENGAI (Angalia sababu)
24
6%
 
Total votes: 378
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#1

This exercise has ended yesterday, 14th November 2019 at 00:00, Tanzania time.

Most of the participants, or generally Tanzania natives are Swahili speakers, it would thus be reasonable to have this information translated in Swahili, as we have done so (see an English version further below).

Form ya kukusanya taarifa ya watakaoshirki katika shindano la kuzipa majina sayarinje na nyota:
https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIp ... g/viewform
Maelezo kuhusu shindano la kutafuta jina la sayarinje:

Kuna sayari zinazozunguka nyota katika anga za mbali (zinaitwa EXOPLANET kwa Kiingereza, na kwa Kiswahili SAYARINJE), zimegunduliwa hivi karibuni na zimeshapewa majina ya kisayansi. Lakini huwa pia zinatambuliwa kwa majina ya kitamaduni.

Katika mwaka huu wa kuadhimisha “Miaka 100 ya Astronomia”, na kwa lengo la kueneza elimu ya Astronomia, kila nchi duniani imepewa sayarinje moja kuipa jina lao. Na Tanzania tumekubaliwa kutafuta jina la sayarinje moja ambayo itatambulisha nchi yetu angani milele.

Sisi kama nchi tunatakiwa tupeleke jina litakalotangaza nchi yetu. Inaweza kuwa jina maarufu kama vile Serengeti, Kilimanjaro, etc. lakini linatakiwa kutafutwa kwa ushindani na kubuniwa kwa kuzingatia tabia ya sayarinje tuliyopewa. Jina litakuwa kwa Kiswahili na la utamaduni wa nchi yetu.

Kwa kuanzia tunahitaji ushiriki wa waalimu na wanafunzi wa mashule (msingi na sekondari) na Vyuo pamoja na taasisi za elimu na makundi ya jamii.

Kujiunga kushiriki katika shindano tuma:
-Jina lako,
- Jina la shule au chuo au taasisi au kundi
Kwa baruapepe:
Assat.Astronomy@gmail.com
au ujumbe mfupi SMS au WhatsApp
0778517009

Mimi ni Dr. Jiwaji, MwanaAstronomia wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Mratibu wa shindano la sayarinje Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Astronomia na Sayansi ya Anga Tanzania (ASSAT) pamoja na (OUT).

For English Audience:

The International Astronomical Union (IAU) has assigned Tanzania, a planet currently identified as WASP-71 b and a star called WASP-71 to run a naming competition. We are asking individuals, groups and organizations, such as schools, clubs, institutions and so on, to suggest names for the planet and the star, and also supply a motivation for their suggestions. More information can be found at http://astrosoc.wixsite.com/nameexoworlds/tanzania.

WASP-71 b is a gas giant exoplanet that orbits a F-type star. Its mass is 1.39 times that of Jupiters, it takes 2.9 days to complete one orbit of its star, and is 0.04622 Astronomical Units (AU) from its star. Its discovery was announced in 2012. See more https://exoplanets.nasa.gov/exoplanet-c ... wasp-71-b/

Naming rules:
Exoworlds naming, stars and planets, Tanzania and Swahili
Exoworlds naming, stars and planets, Tanzania and Swahili
Find more information from attachments both in English and Swahili.

Tarehe za hatua za shindano la kutafuta jina la sayarinje ya Tanzania

• Agosti 1 – Oktoba 15: Majina yatapendekezwa na makundi mbali mbali katika mashule, vyuo, taasisi, na vikundi vya kijamii.

• Oktoba 16: Orodha ya majina 10 yatakayochaguliwa na majaji.

• Oktoba 17 – Novemba 10: Majina yaliyochaguliwa na majaji yatawekwa mbele ya hadhira ya Tanzania kuchagua tatu kati ya hizo wanazopenda zaidi.

• Novemba 12: Tarehe ya mwisho kwa Kamati ya Taifa kuidhinisha jina moja la kupendekeza pamoja na pendekezo la majina mawili kama akiba kwa ajili ya kuwasilisha kwa Umoja wa Kimataifa wa wanaAstronomia (IAU).

• Novemba 13: Majina yanatumwa IAU.

The calendar for the various activities is as follows:

• August 1 – October 15: Names will be proposed by groups in schools, colleges, Universities, institutions, and community groups.

• October 16: Shortlist of 10 names by judges.

• October 17 – November 10: Shortlisted 10 names will be presented for final vote by the Tanzanian public, to vote for the three best names they like.

• November 12: The deadline for National Committees to approve one name proposal for submission to IAU and two backup name proposals.

• November 13: Names sent to IAU.

Naming rules


Please see the official naming rules of the IAU (http://www.nameexoworlds.iau.org/naming-rules) for the full details, but here are the main do’s and don’ts for naming WASP-71b and its star.

TO DO:

• Suggest two names, one for the exoplanet and one for its parent star.
• Use Kiswahili or English or from Tanzanian culture to propose your name.
• Choose things, people, or places of long-standing cultural, historical, or geographical significance, worthy of being assigned to a celestial object.
• Choose names for the parent star and the exoplanet which follow a common naming theme.
• Make sure any other objects in the exoplanetary system can be named using this naming theme.
• Provide a brief explanation (maximum 100 words) why you chose your names.

DO NOT:

• DO NOT Use names which are offensive.
• DO NOT Choose people which died after 1918 or are still alive.
• DO NOT Suggest names of individuals, places or events principally known for political, military or religious activities.

Kanuni za namna ya kutafuta jina

Tafadhali angalia kanuni rasmi za IAU (http://www.nameexoworlds.iau.org/naming-rules) kupata maelezo kamili ya kanuni. Hii itakuongoza vitu gani vya kufanya na vitu vya kukwepa wakati unabuni jina la WASP-71b na nyota-mama yake.

FANYA HAYA:

• Pendekeza majina mawili, moja la sayrinje na moja la nyota-mama yake.
• Unaweza kutumia lugha ya Kiswahii au Kiingireza au utamaduni wa kiTanzania.
• Chagua vitu, watu, au mahala ambapo pana uhusiano wa muda mrefu kwa umuhimu katika utamaduni, historia, au jiografia kuweza kuhusishwa na vitu vya anga za mbali.
• Chagua majina ya nyota-mama na sayarinje yanayofuata dhima moja katika majina.
• Hakikisha vitu vingine katika mfumo wa sayarinje vianaweza kupewa majina kwa kutumia dhima hiyo.
• Toa maelezo mafupi (zaidi kabisa maneno 100) kwa nini umechagua majina hayo.

USIFANYE HAYA:

• USITUMIE lugha chafu au ya kuchukiza.

• USITUMIE watu waliofariki baada ya mwaka 1918 au ambao bado wapo hai.

• USIPENDEKEZE majina ya watu binafsi, mahala au matukio maalum ambayo yanajulikana katika shughuli za kisiasa, kijeshi au kidini.
1 Image 1 Image
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#2

Shindano kwa Watanzania Wote Kutafuta Jina la Sayari-nje ya Tanzania

Tunawakaribisha waTanzania kushindania umaarufu kwa kubuni jina la sayarinje ambayo Tanzania imepewa na Muungano wa Wanaastronomia (wanajimu) wa Kimatafa (IAU) kupendekeza jina la sayarinje yetu pamoja na nyota-mama yake kwa kuzingatia tabia zake pamoja na kuangalia utamaduni wetu hususan kwa lugha ya Kiswahili.

Jiandikishe kwa ajili ya shindano hapa: https://bit.ly/TzGform
Maelezo zaidi kuhusiana na shindano yapo kwenye post #1 hapo juu.
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#3

Yafuatayo ni majina ya SAYARI-NJE na NYOTA-MAMA yaliyopendekezwa na wanafunzi au wanakikundi wengi, sababu za kuchagua hayo majina, na/au maana ya majina hayo. (Nenda kwenye ukurusa wa kupiga kura >>>)
    • Sayari-nje: TANZANITE
      Ni jina la madini yanayopatikana Tanzania duniani kote. Kwa sababu sayari-nje imepatikana hapa nchini tuipe jina hilo maarufu linaloitambulisha Tanzania duniani.
    • Nyota-mama: MPINGO
      Mpingo ni mti maarufu unaopatikana kusini mwa Tanzania na unatoa mbao inayotumika kutengeneza vinyago na vifaa mahususi vya muziki. Uhusiano kati ya Mpingo na Tanzanite kwa sababu kama vile nyota ya Jua ni chanzo cha mabadiliko yote Duniani kwa viumbe na visivyo viumbe kutokana na nuru yake, hiyo basi nyota-mama ya Mpingo ni chanzo cha mabadiliko yanayooneshwa kwa vinyago na muziki kunakotokana na mbao za Mpingo ambapo mbao inawakilisha nuru ya nyota-mama
    • Sayari-nje: CHUNGWA
      Umbo la duara kama sayari, rangi yake kama sayari, mbegu zake na chembechembe zake kuwakilisha idadi ya sayari dunia takriban 3000 ndani yake.
    • Nyota-mama: BOGA
      A) Umbo lake la duara kama la nyota mama-yetu. (B) Rangi yake kama nyota mama-yetu. (C) Mbegu zake kuwakilisha idadi ya majua kuenea ndani yake.
    • Sayari-nje: UHURU
      Kilele cha juu kabisa katika kilima cha Kibo, Mlima Kilimanjaro.
    • Nyota-mama: KIBO
      Kibo ni kilima kuu cha Mlima Kilimanjaro na kina umaarufu wa bila kupingwa barani Afrika na kimataifa. Kilele cha Uhuru kipo Kibo na ni ncha ya juu kabisa Afrika. Vilima vingine katika mlima Kilimanjaro ni Mawenzi kwa mashariki na Shira upande wa magharibi. Sayari-nje ya UHURU ni kama inapita mbele ya nyota-mama yake KIBO. (Zikiwewepo sayari-nje zingine zinaweza kupewa majina kama Mawenzi, Shira, Meru, Hanang, Ol-Donyo Lengai, n.k., katika mfumo kuu utakaoweza kuitwa Kilimanjaro).
    • Sayari-nje: NEUPLADIS
      Sayari yetu ni ya gesi ambayo ni kama nebula.
    • Nyota-mama: LUNYADU
      Kutoka utamaduni wa Kibena. Nyanya dumudumu zinakuwa kama nyota-mama ya sayari-nje yetu.
    • Sayari-nje: ISIMILA
      Hii ni mahala pa kihistoria nchini Tanzania yenye uthibitisho kutokea kwa zamadamu na vilikochimbuliwa vifaa ya enzi ya mawe. Hi inaonyesha mchango wa binadamu katika kuelewa ulimwengu kwa ujumla na kuonyesha umuhimu wa uchunguzi wa ziada wa sayari-nje na kuelewa jinsi ulimwengu wote ulivyoumbika.
    • Nyota-mama: EIBOR-NILIIL
      Kutoka utamaduni wa KiMaasai ina maanisha nyeupe na inang'ara. HI inaendana na aina ya mwanga wa nyota-mama (F8) ambayo inaipa rangi ya manjano-nyeupe na kung'ara kwa sababu ya halijoto kali ya kusababisha mimenyukuo wa myeyungano (fusion reactions) ndani ya kitovu cha nyota-mama hadi kutoa nishati ya joto na mwanga.
    • Sayari-nje: HOMO
      Maana yake ni kitu cha kigeni kinachong'aa angani wakati wa usiku na ni kidogo sana kimwonekano kwa sababu kipo mbali zaidi. Neno hili asili yake ni kabila la Kigorowa au Kimbulu linalopatikana katika Mkowa wa Manyara.
    • Nyota-mama: TSETSEI
      Maana yake ni nyota inayong'aa angani. Pia neno hili asili yake ni kabila la Kigorowa au wambulu walioko mkoani MANYARA.
    • Sayari-nje: CHANDISI
      Utamaduni wa Kimeru. Kitu kikubwa sana kinachozunguka ambacho kinahifadhi vitu vingi vya kitamaduni.
    • Nyota-mama: GIRAG
      Kutoka utamaduni wa kiPemba, ni sawa na Taa ya ajabu inayowaka mwanga mkali unaoweza kuumiza macho, mara nyingi hutumika wakati wa kuabudu mizimu.
    • Sayari-nje: IWAHA
      Utamduni wa Kigogo. Kitu kikubwa ambacho kinaweza kuingizwa ndani yake.
    • Nyota-mama: DEKA
      Kutoka utamaduni wa Kisukuma. Maana yake ni kumi, maana majua kumi yanaweza ingia ndani yake.
    • Sayari-nje: TANZANITE
      (A) Madini ya Tanzaniti ni madini pekee ambayo yanapatikana katika ardhi yetu pekee, na (B) Jina lenyewe la Tanzaniti limetaka kufanana na na jina la nchi yetu, yaani Tanzania, hivyo naona italeta maana sayari hiyo kuitwa sayari ya Tanzaniti.
    • Nyota-mama: KILI
      Kifupisho cha Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu Afrika na kivutio kikubwa duniani na upo Tanzania.
    • Sayari-nje: MBOZI
      Kwa sababu watu wanaosomea mambo ya anga za mbali wana kitu cha kujifunza kupitia kimondo hiki, ni vyema basi hii zawadi au mgeni huyu kutoka anga za mbali tukambatiza jina la sayari mojawapo huko angani.
    • Nyota-mama: OLDONYO-LENGAI
      A) Ni active volcanic mountain hadi leo ambayo inapatikana Tanzania. Kwa vile nyota (jua) utendaji wake wa kazi na mazingira yake yanalingana na volcano, basi ni jina sahihi kabisa kwa hiyo nyota kupewa jina hilo. (B) Itasaidia kuitangaza Tanzania na watalii wengi watapenda kuja kuuona huu mlima.
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#4

Piga kura kuchagua jina linalofaa kwa sayarinje ya Tanzania

Sayarinje ni sayari zinazozunguka nyota ambazo zipo nje ya mfumo wa Jua.

Tanzania tumepewa fursa ya kuipa jina sayarinje mojawapo iliyogunduliwa karibuni.

Wanafunzi wa shule na wanavikundi mbalimbali wameshindanishwa kupendekeza majina ya sayarinje hiyo kwa kufuata asili na utamaduni wa KiTanzania.

Kamati ya Kitaifa ya Sayarinje imeteua majina kumi kati ya yale yaliyopendekezwa ili wewe na waTanzania wengine muweze kupigia kura majina matatu tu kwa kuangalia sababu zilizotumika kupendekeza majina hayo, yakatakayotambulisha Nchi yetu angani milele.

Kupiga kura, nenda kwenye hii tovuti: http://bit.ly/PigiaKuraSayariNje

MWISHO WA KUPIGA KURA NI Tarehe 14 Novemba 2019.

Kwa msaada zaidi tuma ujumbe mfupi (SMS) au ujumbe kwa WhatsApp kwenda namba 0778 517 009 au kwa baruapepe: Assat.Astronomy@gmail.com
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#5

The names of the star and the planet have been published at http://astrosoc.wixsite.com/nameexoworlds/tanzania

The selected names fit a theme of precious natural symbols of Tanzania which can be extended for new discoveries about the WASP-71 system, according to the ExoWorlds National Committee.

Approved Names (Photo Credits: IAU):

Image

Image
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5334
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#6

0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
Locked
  • Similar Topics
    Replies
    Views
    Last post

Return to “News Board”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 2 guests