Most of the participants, or generally Tanzania natives are Swahili speakers, it would thus be reasonable to have this information translated in Swahili, as we have done so (see an English version further below).
Form ya kukusanya taarifa ya watakaoshirki katika shindano la kuzipa majina sayarinje na nyota:
Shindano la Kuzipa Majina Nyota na Sayari-nje/Exoplanets Naming Competition for Tanzanians
Lengo la hii fomu ni kusajili makundi ya watanzania wanaotaka kushiriki katika shindano la kuzipa majina sayarinje ya Tanzania pamoja na nyota yake. Watanzania wamepewa sayari moja na nyota moja ambazo wanatakiwa kuzipa majina ya kiutamaduni wa Tanzania hususan kwa lugha ya Kiswahili. Maelezo, kanuni na taratibu zote kuhusu shindano yametolewa hapa: https://www.tssfl.com/pigia-kura-majina-ya-sayari-nje-na-nyota-za-tanzania-vote-for-tanzania-exoworld-names-mwisho-wa-kupiga-kura-6229Maelezo kuhusu shindano la kutafuta jina la sayarinje:
Kuna sayari zinazozunguka nyota katika anga za mbali (zinaitwa EXOPLANET kwa Kiingereza, na kwa Kiswahili SAYARINJE), zimegunduliwa hivi karibuni na zimeshapewa majina ya kisayansi. Lakini huwa pia zinatambuliwa kwa majina ya kitamaduni.
Katika mwaka huu wa kuadhimisha “Miaka 100 ya Astronomia”, na kwa lengo la kueneza elimu ya Astronomia, kila nchi duniani imepewa sayarinje moja kuipa jina lao. Na Tanzania tumekubaliwa kutafuta jina la sayarinje moja ambayo itatambulisha nchi yetu angani milele.
Sisi kama nchi tunatakiwa tupeleke jina litakalotangaza nchi yetu. Inaweza kuwa jina maarufu kama vile Serengeti, Kilimanjaro, etc. lakini linatakiwa kutafutwa kwa ushindani na kubuniwa kwa kuzingatia tabia ya sayarinje tuliyopewa. Jina litakuwa kwa Kiswahili na la utamaduni wa nchi yetu.
Kwa kuanzia tunahitaji ushiriki wa waalimu na wanafunzi wa mashule (msingi na sekondari) na Vyuo pamoja na taasisi za elimu na makundi ya jamii.
Kujiunga kushiriki katika shindano tuma:
-Jina lako,
- Jina la shule au chuo au taasisi au kundi
Kwa baruapepe:
Assat.Astronomy@gmail.com
au ujumbe mfupi SMS au WhatsApp
0778517009
Mimi ni Dr. Jiwaji, MwanaAstronomia wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Mratibu wa shindano la sayarinje Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Astronomia na Sayansi ya Anga Tanzania (ASSAT) pamoja na (OUT).
For English Audience:
The International Astronomical Union (IAU) has assigned Tanzania, a planet currently identified as WASP-71 b and a star called WASP-71 to run a naming competition. We are asking individuals, groups and organizations, such as schools, clubs, institutions and so on, to suggest names for the planet and the star, and also supply a motivation for their suggestions. More information can be found at http://astrosoc.wixsite.com/nameexoworlds/tanzania.
WASP-71 b is a gas giant exoplanet that orbits a F-type star. Its mass is 1.39 times that of Jupiters, it takes 2.9 days to complete one orbit of its star, and is 0.04622 Astronomical Units (AU) from its star. Its discovery was announced in 2012. See more https://exoplanets.nasa.gov/exoplanet-c ... wasp-71-b/
Naming rules:
Find more information from attachments both in English and Swahili.
Tarehe za hatua za shindano la kutafuta jina la sayarinje ya Tanzania
• Agosti 1 – Oktoba 15: Majina yatapendekezwa na makundi mbali mbali katika mashule, vyuo, taasisi, na vikundi vya kijamii.
• Oktoba 16: Orodha ya majina 10 yatakayochaguliwa na majaji.
• Oktoba 17 – Novemba 10: Majina yaliyochaguliwa na majaji yatawekwa mbele ya hadhira ya Tanzania kuchagua tatu kati ya hizo wanazopenda zaidi.
• Novemba 12: Tarehe ya mwisho kwa Kamati ya Taifa kuidhinisha jina moja la kupendekeza pamoja na pendekezo la majina mawili kama akiba kwa ajili ya kuwasilisha kwa Umoja wa Kimataifa wa wanaAstronomia (IAU).
• Novemba 13: Majina yanatumwa IAU.
The calendar for the various activities is as follows:
• August 1 – October 15: Names will be proposed by groups in schools, colleges, Universities, institutions, and community groups.
• October 16: Shortlist of 10 names by judges.
• October 17 – November 10: Shortlisted 10 names will be presented for final vote by the Tanzanian public, to vote for the three best names they like.
• November 12: The deadline for National Committees to approve one name proposal for submission to IAU and two backup name proposals.
• November 13: Names sent to IAU.
Naming rules
Please see the official naming rules of the IAU (http://www.nameexoworlds.iau.org/naming-rules) for the full details, but here are the main do’s and don’ts for naming WASP-71b and its star.
TO DO:
• Suggest two names, one for the exoplanet and one for its parent star.
• Use Kiswahili or English or from Tanzanian culture to propose your name.
• Choose things, people, or places of long-standing cultural, historical, or geographical significance, worthy of being assigned to a celestial object.
• Choose names for the parent star and the exoplanet which follow a common naming theme.
• Make sure any other objects in the exoplanetary system can be named using this naming theme.
• Provide a brief explanation (maximum 100 words) why you chose your names.
DO NOT:
• DO NOT Use names which are offensive.
• DO NOT Choose people which died after 1918 or are still alive.
• DO NOT Suggest names of individuals, places or events principally known for political, military or religious activities.
Kanuni za namna ya kutafuta jina
Tafadhali angalia kanuni rasmi za IAU (http://www.nameexoworlds.iau.org/naming-rules) kupata maelezo kamili ya kanuni. Hii itakuongoza vitu gani vya kufanya na vitu vya kukwepa wakati unabuni jina la WASP-71b na nyota-mama yake.
FANYA HAYA:
• Pendekeza majina mawili, moja la sayrinje na moja la nyota-mama yake.
• Unaweza kutumia lugha ya Kiswahii au Kiingireza au utamaduni wa kiTanzania.
• Chagua vitu, watu, au mahala ambapo pana uhusiano wa muda mrefu kwa umuhimu katika utamaduni, historia, au jiografia kuweza kuhusishwa na vitu vya anga za mbali.
• Chagua majina ya nyota-mama na sayarinje yanayofuata dhima moja katika majina.
• Hakikisha vitu vingine katika mfumo wa sayarinje vianaweza kupewa majina kwa kutumia dhima hiyo.
• Toa maelezo mafupi (zaidi kabisa maneno 100) kwa nini umechagua majina hayo.
USIFANYE HAYA:
• USITUMIE lugha chafu au ya kuchukiza.
• USITUMIE watu waliofariki baada ya mwaka 1918 au ambao bado wapo hai.
• USIPENDEKEZE majina ya watu binafsi, mahala au matukio maalum ambayo yanajulikana katika shughuli za kisiasa, kijeshi au kidini.