Ushauri wangu kwa Wanaosoma, Wanaotafuta ajira, Walioajiriwa na Waliojiajiri

This sub-platform is all about risk taking functions. Help others to learn how to develop unique business ideas, acquire resources and dare for success!
Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Leo nimejionea wasiwasi mkubwa na mashaka yaliyoonyeshwa na baadhi ya wafanyakazi kuhusiana na hatma zao baada ya kitendo cha wao kutokupata mishahara huku wengine wakipata. Swala hili linasemekana kusababishwa na mfumo mpya wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa serika kupitia BOT ujulikanao kama "GSPP".

Kutokana na hali hiyo, ndipo nilipopata wazo la kuandika habari hii.

Hakuna watu wapo kwenye hatari na mashaka kuhusiana na maisha yao kama wafanyakazi walioajiriwa iwe na serikali au sekta binafsi. Hatari hii wengi huwa hawaioni wala kujifunza hata pale wenzao wanapokumbwa nayo. Hatari yenyewe ni kwamba, "lolote laweza kutokea kuhusiana na ajira zao". Mfano wa mambo yanayoweza kutokea kuhusiana na ajira ni kufukuzwa, kuachishwa kazi (kustaafishwa au kwa sababu yoyote ile). Serikali au mwajiri mwingine yoyote hawezi kutabirika, na kitendo cha wewe kwenda kazini kila siku na kurudi bila kuona dalili zozote za mwisho wa kazi yako isiwe kigezo cha kukufanya wewe ubweteke.

Kuna namna ambapo kazi yako inaweza kuzima haraka mno kuliko unavyodhani. Jiulize, wafanyakazi kama wale waliokutwa na kashfa, mfano za madini, hatma yao ni nini? Sina maana kwamba kwa sababu wewe unafanya kazi kwa weledi na kwa kufuata taratibu zote, basi upo salama! Kuna "uncertainties" nyingi sana ambazo zinaweza kumkumba mfanyakazi, mfano linaweza kuzuka jambo kazini wewe ukakumbwa nalo hata kama huhusiki na likakuchukua kama mkondo wa maji. Wafanyakazi watanielewe namaanisha nini hasa ukizingatia mazingira halisi ya kitanzania kazini. Hivi umeshawahi kuona baadhi ya watu kazini wanatamani mambo yako yakwame wafanye sherehe? Yaani, kama wana uwezo wa kukutafutia zengwe lolote lile watalitafuta ilimradi likupeleke na maji? Hii ni moja ya "scenario" tu ambapo unaweza kujikuta jana jioni umetoka kufanya vema kazi yako, leo asubuhi na mapema kazi huna!

Nia ya maelezo yangu hapo juu ni kwamba, umejipangaje iwapo hali yoyote inayofanana na hiyo itakutokea?

Je, kama mshahara ukikosekana siku moja (sisemi huna haki kupata mshahara au ni sahihi kucheleweshewa) tu tunahaha, je ukiachishwa kazi kwa kushtukiza?

A. Ushauri wangu kwa wafanyakazi walioajiriwa na serikali au sekta binafsi (hii ni kuanzia housegirl na kuendelea)

0. Kama unataka kuendelea kuajiriwa na unaipenda sana kazi yako, hakikisha una weledi na ujuzi hasa kuhusiana na hiyo fani yako. Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba, weledi na ujuzi (siongelei ufaulu wako kwenye makaratasi - naongelea utendaji "in the real world") wako usio na shaka ndio utakulinda, kwani hata mwajiri akitaka kukufukuza (hasa kwa sababu zisizo za msingi sana) analiona pengo lisilozibika na kufikiria mara mbili mbili. Weledi na ujuzi ulionao ambao ni zaidi ya wastani, utakupa pia uwezekano wa kuajirika kwingine kirahisi endapo utaachishwa kazi ya awali kwa sababu zozote zile.

Kuwa makini weledi na ujuzi wako usikufanye uwe na kiburi bali uwe msaada na kimbilio. Mfano, kama wewe unajishughulisha na mambo ya takwimu, endeleza maarifa yako, jua kutumia "exceptionally" "tools" kama vile excel spreadsheets na zingine ambazo labda ndio muhimu kwenye kazi yako. Gundua tools na njia mpya na zitumie kuboresha na kurahisisha kazi - ukifanya kitu mpaka boss anajiuliza huyu jamaa ni mchawi au!!?

1. "Diversify your skills" - Ni vizuri sana kuwa na maarifa mengine ya ziada ambayo yatakupa fursa ya kuzalisha, kutoa huduma au kutumikia sehemu na kuingiza kipato zaidi ya ile kazi ya msingi unayoifanya - ambayo mara nyingi ndiyo uliyoisomea darasani. Maarifa haya ya ziada, hasahasa yalenge kukufanya ujiajiri.

Mara moja unapoanza kupata haya maarifa mapya anza kuyafanyia kazi taratibu huku ukijiendeleza zaidi. Hakikisha hayo maarifa mapya yanaanza kukutengenezea fursa.

Hebu jiulize, mfano wewe ni mwalimu wa somo la uraia shule ya msingi au wewe ni secretary ofisi fulani na kazi yako kubwa ni kutembea na mafaili au wewe ni mwanapropaganda wa chama fulani cha siasa; je, ukifukuzwa kazi? Au serikali ikasema kuanzia leo somo la uraia shule ya msingi tumelifuta (mwalimu), utaenda wapi kama huna maarifa mengine? Hata kama kuna uwezekano wa kutafuta kazi, je, utaipata kirahisi? Hasa ukizingatia ni raia wangapi hawana kazi? Pengine hata umri wako utakuwa umeenda na huajiriki tena!

2. Kuwa na project/biashara nyingine ambayo unaweza kuiendesha sambamba na kazi yako bila kusababisha mwingiliano wa kiutendaji na ajira rasmi. Pamoja na kuwa na hiyo biashara/project, ni muhimu kutafuta maarifa na kuendelea kujiupdate ili kuhakikisha kuwa project hiyo ni endelevu. Endelevu sina maana kuwa kwa kipindi utakachoishi wewe, bali hadi kwa vizazi vyako vyote vijavyo.

3. Hakikisha biashara/project/maarifa yako yanaanza kukupa nafasi ya kuona ajira ni kitu cha ziada (sina maana usitimize wajibu) kabisa, bali namaanisha hata ikitokea huna hiyo ajira, maisha yataendelea. Ijengee familia yako mtazamo wa kujiajiri na sio kuajiriwa, kuanzia mtoto wako mdogo anayezaliwa na kuendelea. Usipoweka hiyo legacy, tarajia kuona watoto na vizazi vyako kuendelea kuthamini zaidi kuajiriwa kuliko kujiajiri, na tarajia kuumia kwa kuona kizazi chako kutembea na bahasha kila ofisi kuomba kazi, kuyumba kwa kufuata na kusikiliza kila aina ya ushauri na habari inayohusiana na ajira na kukosa mwelekeo kimaisha.

4. Baada ya kutimiza hayo hapo juu, hasa 1-3, sasa panua wigo na ajiri wengine.


B. Ushauri wangu kwa wanaosoma na wanaotafuta ajira

Ni muhimu kuelewa na kujiridhisha kwa nini unasomea kitu fulani. Ili uweze kupata ajira haraka mara tu umalizapo masomo? Ili uje kutumia elimu yako kutatua tatizo/matatizo fulani? Ili upate vyeti umefuzu kozi fulani? Ili ....?

Kama lengo lako la kusoma ni kutafuta ajira au kujiajiri, vyote hivi vinataka uhakikishe unasoma na kupata ujuzi na weledi katika fani husika. Soko la ajira na hata utendaji vitategemea sana na uwezo wako, sio tu kwa kufaulu na kuwa na A's au kushinda interview kwa kumeza vitu na kuvitema bila hata kuvielewa wewe mwenyewe, bali uwezo wako wa kutafsiri elimu uliyonayo katika vitendo.

Ni jambo la kushangaza sana kila leo nakutana na watu wengi wanaojinadi kusomea fani fulani, lakini utendaji au uwezo wao ni chini ya kiwango. Ingawa sitarajii mtu aliyetoka mfano chuo awe na uwezo wa kiutendaji kama mtu aliyebobea kwenye fani husika, lakini ni lazima uonyeshe kivitendo kuwa wewe ni graduate wa fani fulani. Kupata elimu ya kutatua matatizo katika ulimwengu halisi, sio swala jepesi wala lelemama na mara nyingi ni "painful process", vinginevyo, kila mtu angeweza kuipata na kuwa na ujuzi na maarifa yanayotakiwa kirahisi.

Kabla ya kuamua ni kitu gani usome na ni namna gani unataka kutumia elimu yako, ningependa usome makala hizi mbili:

1. Future Predictions: Article by Dr. Robert M. Goldman

2. Three Essential Skills for Success in Future Job Market

Kama lengo lako ni ajira, lazima uwe na uwezo wa kuona soko la ajira inayotokana na taaluma fulani litakuwaje hapo baadaye. Hii haina maana fani ambazo zina mahitaji makubwa leo zitaendelea kuwa hivyohivyo siku za usoni, na fani ambazo zina uwezekano finyu wa kuajiriwa leo zitaendelea kuwa hivyo ingawa kunaweza kuwa na "some exceptions". Lazima uwe na "scientific base" na kufanya "reasonable analysis" kupredict "future job trends".

Vichekesho huwa vinaanza na aina hii ya wasomi, mfano mzuri ni hawa ndugu zangu, unakuta kasoma labda computer science, computer engineering, information technology au software engineering/developing, sasa mwuulize umesomea nini? Kwanza atakujibu "Mimi ni IT", wengi hawawezi kufafanua na kukueleza zaidi ya kuwa wao ni IT!

Anyway, wewe ni IT! IT na fani zinazohusiana nayo ni "rapid evolving fields", ni moja ya maeneo yenye "avenues" nyingi kwa sababu applications zake ni karibu katika kila eneo la maisha kwa sasa.

- Sasa inakuwaje umesomea mojawapo ya fields nilizozitaja hapo juu, lakini huwezi kufanya au kuonyesha kwa vitendo japo kitu kidogo cha Ki-IT, kama vile kutengeneza desktop au mobile app, system ya kusolve tatizo fulani, etc.,?

- Inakuwaje wewe ni IT kwa mjibu wako, lakini linapokuja swala la sisi kutaka kuona maarifa yako, uwezo hautofautiani na mtumiaji mwingine yeyote wa kawaida wa kompyuta/simu, anayetumia kusurf internet na blogs, kuchat kwenye social media/platforms na labda sanasana kutumia baadhi ya simple applications tena kwa shida?

- Umeapply sehemu kibao kutafuta kazi, labda huu ni mwaka wa 2, inakuwaje application yako ya miaka 2 iliyopita ni sawa na ya leo? Yaani wewe hakuna ulichokifanya tangu ugraduate kuonyesha kwamba wewe ni IT kweli, CV ipo hivyohivyo (sina maana upachike vitu kwenye CV hata ambavyo huvijui - na hiyo ni kawaida sana kwa watu wengi hasa watanzania), nina maana in real world kuna app, system, software au solution yoyote ya ki-IT umeimplement?

- Watu wengi wanaojiita IT wanabaki kutengeneza blogs, kutumia muda mwingi kupost umbea mitandaoni kama vile picha na habari za wasanii au watu maarufu - lengo labda ni wapate fedha kupitia Google AdSense, hasa kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanapenda umbea na habari za ovyoovyo, basi wengi wamefanya hayo mambo kama ajira rasmi!

Ni jambo la aibu na inabidi vijana wabadilike. Kazi kama za kupost umbea zinaweza tu kufanywa na housegirl aliyemaliza darasa la 7 au hata 4 ukimwelekeza na akawa anaingiza hela kupitia matangazo, kama ni muhimu au lazima, unachohitaji tu ni laptop/desktop/tablet/simu, internet na kumpa maelekezo kidogo, lakini hiyo kamwe haiwezi kuwa kazi rasmi ya I-technologist.

Hapo juu, nimetolea mfano kwenye nyanja moja, lakini hili tatizo la vijana kutozitendea elimu zao haki lipo katika fani zote.

Kama wewe ni computer technologist au computer scientist au muhitimu wa fani yoyote, kwa namna yoyote, fursa zipo nyingi:

1. Hakikisha unatumia na kuboresha maarifa yako kila kukicha - usisubiri kutumia maarifa yako siku utakapoajiriwa. Ukisubiri mpaka ajira hakika utayapoteza na hata uwezo wa kutetea ulichokisomea unaweza kupotea kabisa. Kupractice na kujiendeleza kwenye fani yako kutakuweka up-to-date na maarifa mapya na namna mpya za utendaji, kwa namna hiyo lazima uwe tofauti na wengine. Hali hii itapelekea kuajiriwa au kujiajiri kwa urahisi zaidi.

2. Tafuta sehemu au jambo ambalo litakufanya utumie maarifa yako, hata kama hulipwi - ni njia ya kujifunza utendaji halisi na kujionea tofauti kubwa iliyopo kati ya "theory" na "practice".

3. Ungana na watu wengine wenye nia na maarifa kama yako kuanzisha mradi/project/biashara inayotumia elimu uliyosomea.

4. Kuwa na nidhamu na "focus" katika makubaliano na utendaji, watu wengi hasa vijana hawana nidhamu wala focus, wanaongea hili na wanakubaliana, baada ya dakika mbili wamesahau na hawakumbuki makubaliano, achilia mbali utekelezaji.

5. Tumia muda wako vizuri, hasa kufikiria na kufanya mambo ya maana, hata kama hayana uhusiano na kile ulichosomea, hii itaendelea kukujengea uwezo wa kuendeleza na kutumia akili yako kwa usahihi. Matumizi sahihi ya akili ndio ambayo hupelekea "creativity na innovation". Itakupa uwezo wa wewe kujiajiri, kutatua matatizo yako binafsi na kupata fursa ya kutatua matatizo ya watu wengine.

6. Ni muhimu kuilinda afya yako kwa gharama zozote. Epuka ulevi, sigara, madawa ya kulevya na ngono. Ukientertain mojawapo ya hizi tabia, uwezo wa wewe kutimiza au kutekeleza 1 - 5 hapo juu, ni kwa miujiza.

C. Ushauri wangu kwa waliojiajiri

1. Endeleeni kujiajiri, lakini msisahau kuongeza maarifa mapya na ujuzi vinavyohusiana na sector zenu. Someni trends na mielekeo ya biashara/projects/kazi zenu. Kuweni macho na mazingira na mabadiliko yoyote yanayoweza kuathiri kazi zenu na chukueni hatua stahiki mapema kukabiliana na hali halisi. Mnaweza msikosee jambo lolote katika utendaji wenu lakini bado mkapotea vilevile! Mkumbukeni Nokia CEO, "we didn’t do anything wrong, but somehow, we lost".

2. Kama wewe ni mjasiriamali, anza kukua na kufikiria kuwa investor. Tumia rasilimali zako, elimu, uongozi na usimamizi wako kukuza kampuni/biashara/mradi. Fikia kiwango cha kutumia mali na rasimali watu kuendesha kazi yako. Lipa wafanyakazi vizuri sana ili wawe na motisha wa kufanya kazi kwa weledi na ubunifu zaidi na zaidi, wafanye wafanyakazi rafiki zako na wajisikie kufanya kazi kwako ni kama nyumbani kwao. Lakini jua aina za business risks na namna ya kuziepuka: Types of Business Risks
0
Post Reply

Return to “Entrepreneurship, Business, Economy”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests