• Active Topics 

Tanzania software engineers/developers GitHub Community

Are you studying or working? What is your lifelong career ambition and why? Why have you chosen what you are studying and who do you want to be?
Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Habari wadau,

Nina wazo kuwa watu wote ambao wanapenda kujifunza namna ya kudevelop applications mbalimbali - desktop, mobile, cloud au vyovyote vile na wale ambao wamebobea katika kudevelop software mbalimbali wafungue community public repositories GitHub kwa ajili ya kujifunza na kushirikiana namna ya kudevelop applications. Hii itawezesha developers waliobobea kuwa mentors kwa wengine na wale ambao wanajifunza hata kama kuanzia hatua za mwanzoni kabisa kufundishwa na kujifunza.

Haihitaji kuanza kudevelop app au system ambayo ni complicated sana, bali kuanza tu kujifunza basics na kuendelea hatua kwa hatua.

Kuanza kwanza kwa kufahamu matumizi ya Git na GitHub itakuwa ndio msingi wenyewe.

Nina amini kuna watu wengi humu wenye nia ya kufundisha, pia wapo wengi wenye nia ya kujifunza.

Hii ni njia nzuri ya kutengeneza online community ya developers/software engineers hasa wa Kitanzania.

Usije na wazo kwamba nilishajaribu ikashindikana na malalamiko mengine ya namna hiyo, njoo na wazo la namna gani hii online community ya developers ninayoifikiria mimi inaweza kuwa successful na sustainable.

Kuwa na online community ya developers sio tu ni njia ya kujifunza na kufundishana, bali itatoa ajira kwa watu kwa sababu watu wataona uwezo wako, na pindi mtu au kampuni itakapohitaji app au maarifa yako, basi itakuwa ni nafasi nzuri ya wewe kupata tender/ajira.

Baadaye tutakuja kuwa na events kama BootCamps, coding competitions - na kutoa zawadi mbalimbali kumotivate developers na wale wanaojifunza, get together, na ikiwezekana digital lab yetu - yaani sehemu ambapo tutaweza kuonana physically kwa ajili ya mihadhara, developments, hands-on training/mentorship, kusolve challenges mbalimbali na kadhalika.

Tuache kulalamika, kama kweli tupo serious, "let's take an adavantage of an upcoming industrial sector in Tanzania" - kumbuka kama nchi itaendea kuwa ya viwanda, kutakuwa na massive need ya applications, software na systems mbalimbali kwa ajili ya kuendesha viwanda - kuanzia kwenye operations, monitoring, control, management, production, service provisions, etc.,.

Nasubiri michango na maoni yenu.
2 Image
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5212
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#2

Here is a Github account we have created for software developers, programmers, coders, e.tc.,

https://github.com/TSSFL
1
1 Image
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
Post Reply

Return to “Study, Work & Career”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests