• Active Topics 

Ni aibu sana kwa Taifa kulilia au kutegemea misaada kutoka nchi za Ulaya, US, China au kutoka kwingineko

This subforum is about Africa continent development policies, plans and strategies, including but not limited to Education Policies, Poverty Reduction Strategies, Economic Policies; approaches used to implement them, success and failures; and what Africa need to do to become an industrialized and a developed continent.
Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 164
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Mara kadhaa nimekuwa nikishangazwa na watu wengi wakililia misaada kutoka nje ya nchi au kunyong'onyea, kusikitika na kuchukulia kama ni pigo kubwa kwa maendeleo ya Taifa kama nchi ikikosa misaada kutoka Ulaya, Marekani au Uchina au wakati mwingine kutoka nchi zingine Africa.

Nimeshawahi kusikia watu wakiongea au kuandika hivi "CHADEMA/wapinzani wangefurahi sana kama nchi ingekosa misaada au "CHADEMA/wapinzani wangefurahi sana kama wahisani wangesitisha misaada", na kauli zingine za namna hiyo.

Kauli za namna hiyo na zingine zinazofanana nazo, za kungang'ang'ania au kulilia misaada na kujisifia kupokea au kupata misaada zitaifanya Africa ikiwemo Tanzania kuzidi kudidimia, achilia mbali kuendelea. Ukitaka kujua kama nchi inaendelea au inadimimia, linganisha au fanya "Benchmarking" na nchi zingine ambazo kwa miongo kadhaa iliyopita zilikuwa sawa na Tanzania au zilikuwa hata nyuma ya Tanzania kimaendeleo (Naongelea maendeleo, tena endelevu, ya Kiuchumi, Kielimu, Kisayansi, Kiviwanda, Kibiashara, Kiafaya, Kiutamaduni, nk). Pia linganisha rasimali ilizonazo nchi, na kujaribu kujiuliza, hizo rasilimali ingekuwa nazo nchi nyingine iliyopiga hatua kimaendeleo, kwa mfano, Singapore, Korea ya Kusini, China au USA ingekuwa wapi hivi sasa?

Leo, tuwasikilize wanauchumi na wachambuzi kadhaa wa maswala ya uchumi na maendeleo, wakijaribu kuonyesha waziwazi kuwa Afrika ikiwemo Tanzania, haviwezi kuendelea kamwe iwapo mambo kadhaa muhimu na hatua kali za makusudi "radical changes" hazitachukuliwa, ikiwemo kuachana na kukataa katakata misaada ambayo ndiyo chanzo kimojawapo kilicholemaza na kudumaza harakati za maendeleo barani Afrika - kuwa tegemezi ni kilema kibaya mno.

Wachambuzi hawa ni pamoja na Dr. Dambisa Moyo, "Zambian economist" na msomi mashuhuri, aliyebobea kwenye mambo ya "Global economy". Dr. Moyo amemaliza Masters degree yake Harvard University na PhD kutoka Oxford, ni moja kati ya watu 100 "top 100" mashuhuri na wenye ushawishi mkubwa duniani, ametembelea karibu nchi 100 duniani kwa ajili ya kutoa ushauri wa kiuchumi kwa mataifa, taasisi na kampuni, kwenye nyanja za biashara, uchumi, ujasirimali, teknolojia, nk.

Dr. Moyo ni mwandishi wa vitabu vitatu maarufu duniani, "Dead Aid, Why Aid Is Not Working and How There is Another Way for Africa, How the West Was Lost: Fifty Years of Economic Folly – And the Stark Choices that Lie Ahead and Winner Take All: China’s Race for Resources and What It Means for the World."

Katika kitabu chake maarufu na ambacho kiliuza nakala nyingi sana, Dead Aid, kuna hii excerpt:

"Giving more aid to Africa over the course of the years did not alleviate poverty, instead it kept the economy crippled with governments asking for more aid. This fluke made a cycle of aid giving which resulted in nothing productive and it has not been used to solve the immediate problems and the money is not being used to make businesses sustainable in Africa"

Hapo awali, Dambisa Moyo alikuwa consultant Golman Sachs Group na mwanauchumi wa Bank ya Dunia.

Sasa ana majukumu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye Board ya Wakurugenzi ya Barrick Gold (Nikiandika ACACIA nitaeleweka vizuri zaidi):

"Dambisa has earned a strong reputation as a top-tier opinion former and trusted advisor on Macroeconomics, Geopolitics, Technology and Millennial themes. She is a Board member of Barclays Bank, Barrick Gold, Chevron and Seagate Technologies. She holds a PhD in Economics from Oxford, a Masters from Harvard, and is recognized for fresh and innovative ideas as the Author of three (3) New York Times Bestselling Books:" -Biography | Dambisa Moyo

Sasa sikiliza interviews za BBC (HardTalk) na Dr. Moyo, na TED Talk ya Dr. Dambisa Moyo:







Sio mbaya tukimalizia kwa kuwasikiliza na hawa:





Kinachotakiwa Tanzania na Africa sio misaada ya hela au vitu, bali ni sisi wenyewe kufanya juhudi za kutafuta maarifa/ujuzi/elimu ambavyo vitatupa uwezo wa kufanya chochote tunachotaka.
1
1 Image
Post Reply

Return to “Africa Development Policies, Strategies and Plans”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests