Kati ya Yesu Kristo na Muhammad, ni Yupi Anayekushawishi Kuwa ni Mtume wa Mungu?

Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Tufanye (tuassume) una akili timamu, una uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa ufasaha.

1. Umeishi nyakati za Yesu Kristo, ukakutana naye, ukaona na kusikia anayoyafanya, ukalinganisha mambo na habari zake kwa kusoma Biblia ambayo iliandikwa miaka mingi kabla ya ujio wake kwa nyakati tofauti na watu tofauti walioishi sehemu mbalimbali/tofauti.

2. Baadaye akazaliwa Mtume Muhammad, ukabahatika kushuhudia maisha yake ya ukuaji, akilelewa na mjomba wake Abu Talib (mwenye ubini na baba yake). Siku za usoni katika ukuaji wake ukaanza kushuhudia mara kwa mara akijitenga na jamii hasa nyakati za usiku na kwenda katika pango la Hira lililoko mlima Jabar al-Nour katika sehemu ijulikanayo kama Hejez (kama kilomita 3 hivi kutoka Mecca) magharibi mwa Saudi Arabia ya leo. Madai ya kujitenga kwake na kwenda pangoni ni kwa lengo la kuswali.

Baada ya kufikisha miaka kama 40 hivi, Muhammad akaibuka ghafla siku moja na kudai kuwa ametembelewa na Malaika Gabriel akiwa katika pango la Hira na kupewa mafunuo (revelations) kutoka kwa Mungu. Miaka mitatu baadaye (mwaka wa 610 kwa mjibu wa Kurani), akaanza kuhubiri hayo mafunuo hadharani (kupitia mihadhara).

Tufanye pia unafahamu maisha na historia ya Muhammad kama ifuatavyo:

Katika kuhubiri mafunuo aliyodai kupewa alikumbana na upinzani mkali sana yeye pamoja na wafuasi wake kadhaa waliomfuata kutoka kwa baadhi ya Wamecca. Kitendo hicho kilimfanya akimbilie Madina/Medina, kama mwaka wa 622 hivi. Hiki kitendo cha Muhammad kukimbilia Madina kinajulikana kama "Hijra" na ndio mwanzo wa kalenda ya kiislamu "Hijri".

Akiwa Madina, Muhammad aliunganisha makabila chini ya katiba, ijulikanayo kama Katiba ya Madina. Pamoja na kuwa Mohammad alikimbilia Madina, uhasama kati yake na Wamecca uliendelea, na mara kadhaa palitokea ugomvi au msuguano dhidi yake na makabila ya Mecca. Mwaka 629, Muhammad alikusanya wanajeshi (wafuasi wake) wanaokadriwa kuwa kama 10,000 hivi na kuivamia Mecca. Uvamizi ulikuwa ni wa nguvu kubwa hasa kwa wakati huo, na Muhammad aliweza kuikamata Mecca bila upinzani mkali, kwa umwagaji damu kiasi.

Mwaka 632, Muhammad aliugua na kufa, lakini kabla ya kifo chake alihakikisha karibu jamii yote ya Peninsula ya Arabia (Yemen, Oman, Qatar, Bahrain, Kuwait, Saudi Arabia, UAE na sehemu za Jordan na Iraq) ilishageuka kuwa waislamu.

Mafunuo/mafundisho haya, yajulikanayo kama "ayah", ambayo waislamu huchukulia mpaka leo kama Neno la Mungu, ndiyo yale ambayo Muhammad alidai kupokea kutoka kwa Mungu kupitia Malaika Gabriel, na ndiyo yanayotengeneza aya za Kurani, ambayo ndiyo msingi wa dini ya Kiislamu. Kimsingi, Muhammad aliunganisha waarabu karibu wote na baadhi ya waajemi na kusisitiza kuwa mafundisho yake, matendo yake, imani yake, na Kurani yake vinakuwa ndio msingi wa imani ya Kiislamu.

Katika kuhubiri kwake alisisitiza kuwa yeye ni mtume wa mwisho wa Mungu kuja duniani, na kuwa amekuja kutimiliza mafundisho ya msingi ya akina Adam, Abraham, Mussa, Yesu Kristo (Nabii Issa) na manabii wengine katika Kurani.

Swali:

Je, baada ya wewe kuwa umewashuhudia Yesu Kristo na Muhammad, ni nani ambaye angeweza kukushawishi kuwa ndiye mtume wa kweli wa Mungu na kumwamini?

Je, Uislamu sio project tu kama ilivyo projects zingine nyingi?
0
Post Reply

Return to “Other Community-Based Discussions”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests