• Active Topics 

Hata wazungu kutoka nchi mbalimbali za Ulaya wanakimbilia USA

Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja kupitia skype jana, yeye anaishi Boston, USA. Sasa katikati ya maongezi yetu, kuna jamaa kadhaa ghafla wakaingia ndani kwake, akaniambia samahani, ngoja niwasikilize hawa jamaa, mimi nikawa nimehang kwa muda kidogo skype lakini nawaona na kuwasikiliza yeye na hao jamaa wakiongeaongea, wlikuwa kama watano hivi. Baada ya dakika labda 5 hivi, mazungumzo yakawa yameisha, mimi na yeye tukaendelea kupiga story.

Nikamwuuliza hao ni akina nani? Akajibu, ni jirani zangu, ni jamaa wa Portugal, Italy na Spain na mwingine Mmarekani, wamekuja kunishtua, kwa ajili ya event fulani ambayo itaanza muda si mrefu, nami natakiwa kuhudhuria.

Katika story zetu, akawa ananiulizia issue za Bongo, matukio na mambo ya kawaida ya kila siku. Sasa baadaye kidogo tukawa tunaongelea hali halisi ya maisha huku Bongo na huko USA. Jamaa alinishtua kwa kuniambia kuwa sehemu nyingi sana duniani, maisha ni magumu sio Africa tu. Mara nyingi wazungu wamekuwa wakituaminisha kuwa sisi waafrika ndio tuna maisha magumu na ya dhiki kuliko wao, lakini, ukweli nchi nyingi sana za ulaya watu wana hali mbaya sana, alisema. "Uliwaona hawa jamaa waliokuwepo hapa, kati yao kuna mtu kutoka Italy, Spain na Portugal, hawa jamaa walikuja huku kama kutembea au kusalimia ndugu au rafiki zao, lakini wanakuambia hawarudi nchi zao hata iweje".

Amedai kuwa kuna maelfu ya watu kutoka nchi nyingi za ulaya, zikiwemo England, Spain, Uturuki na Italy wakija hapa USA wanang'ang'ania kuishi hata kama kwa vibarua vya kuungaunga kwa sababu hali kwenye nchi zao ni tete. Wengi sana tu na wanakuja hapa USA kwa njia haramu, cha ajabu husikii wakisemwa.

Sikutegemea nchi kama Italy, Spain na England watu wao kukimbilia USA kama ambavyo imekuwa inajulikana wanaokimbilia huko ni waafrika tu.

Amesema watu kama Wamexico, wanakata mbuga hata kwa mguu ili mrdi waingie USA. Wahindi na Wachina ambao huku kwetu wanaonekana ni wajanja wapo tayari hata kulala ndani ya jela za Marekani, kurudi kwao hawataki, ni kama wanaenda kufa.

Ameongeza kuwa Marekani kuna fursa lakini zinategemea na mambo kadhaa: bahati na elimu. Bahati ni kama ukiajiriwa sehemu hata kama una elimu ndogo ukaifanya kazi yako kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa, kampuni inakupenda na kukung'ang'ania. Kuhusu bahati amenitolea mfano wa mtanzania mmoja anayelipwa $400 kwa siku wakati elimu yake ni ya darasa la saba Tanzania.

Kuhusu kupata kazi kwa kuwa na elimu, amesema kuwa sio kila elimu inalipa - yaani inaweza kukupatia kazi japo kwa urahisi isipokuwa kuna "skills" ambazo ukiwa nazo uwezekano wa kupata kazi USA ni mkubwa. Kuhusu kupata kazi kwa njia ya elimu, amenipa mfano wa Mtanzania aliyeajiriwa na kampuni moja hapo Boston kama software engineer. Sekta zingine kadhaa za science pia zinalipa na bado wataalamu wake USA wanahitajika pamoja na lundo la wasomi wanaograduate kila mwaka nchini humo.

Amehitimisha kwa kusema sio kila nchi ya Ulaya ni ya kukimbilia.

Nimeona niandike ili kuwasaidia wale wanaotaka kujirusha nje ya nchi waangalie ni wapi wataangukia, sio tu ilimradi Ulaya.

NB: Nilimwuuliza kuwa, mtu ambaye hajasoma, hana ndugu USA au rafiki aliyemwalika kwenda kumtembelea, au mchumba hata kama ni feki, anaingiaje USA? Atapewa visa kwa ajili gani? Alinipa jibu fulani ambalo ndio lilihitimisha mazungumzo yetu, kwamba kwa mtu kama huyo, options zipo nyingi ila ya kwanza kwa sasa ni kuwa na "passport ya Libya au Sudan".

Takwimu za watu kutoka nchi mbalimbali wanaokimbilia USA

Image

Soma zaidi:

https://www.quora.com/How-many-British- ... in-the-USA

http://www.telegraph.co.uk/news/2017/06 ... est-local/

http://www.bbcamerica.com/anglophenia/2 ... to-america

https://www.verdict.co.uk/which-compani ... of-brexit/

http://news.bbc.co.uk/2/hi/uk_news/magazine/4226949.stm

http://www.independent.co.uk/news/busin ... 95486.html

http://www.washingtontimes.com/news/201 ... on-france/
0
Post Reply

Return to “Other Community-Based Discussions”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests