• Active Topics 

Dr. Shika Ametisha Lakini Hafikii Hata 1/10 ya Kitendo Alichowahi Kukifanya Morris Sankuu

Are you a good storyteller/writer, based on facts or created from imagination? Why not write here for us?
Post Reply
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#1

Pamoja na Dr. Shika kugonga headlines kwa kitendo chake cha kutoa ahadi hewa za kununua nyumba za Lugumi, hafikii hata 1/10 ya kitendo alichowahi kukifanya Msomi Morris Sankuu. Sankuu alizuka miaka ya 1970 kijijini kwetu na kudai kuwa ametokea masomoni Moscow, Urusi. Huyu jamaa alikuwa kila wakati anatembea na matabu makubwa kuliko Dictionary ile ya Kiingereza ya Oxford. Ilikuwa akikutana na mtu mwenye viashiria vya kuwa msomi au mwanafunzi anamwapproach kwa kiingereza, na kuzusha mdahalo wowote naye, lakini kiingereza chake kilikuwa ni kigumu hata cha Prof. Lumumba hakioni ndani. Huyo msomi muda wote alikuwa smart, kuvaa kwake ilikuwa ni mwendo wa suti, tai na viatu aina ya raizoni (enzi hizo raizoni huigusi).

Sasa siku moja alienda kwa uongozi wa kijiji na kuweza kuwashawishi viongozi waitishe mkutano ana mambo muhimu sana anataka kuongea na wananchi. Kutokana na wito wake na approach yake, viongozi wa kijiji chetu walimuunga mkono na kukubaliana kuwa badala ya mkutano uwe wa kijiji, waitwe wananchi kutoka kata nzima. Kwa hiyo ilikuwa ni mshikemshike wa harakati za viongozi wa vijiji kuwaalika wananchi wao. Issue yake ilipewa kiki ikakua zaidi, na kusambaa mpaka eneo la wilaya na mkoa. Nakumbuka majira hayo kulikuwa na mbio za mwenge. Viongozi ngazi za mkoa na wilaya waliazimia kuwa ufanyike mwaliko wa Rais, kwenda kumsikiliza Sankuu kijijini kwetu na sehemu hiyo iwe ndio hitimisho la mbio za mwenge.

Rais (Baba wa Taifa) aliitikia wito kwa mikono miwili. Baada ya mwitikio zilianza shamrashamra za maandalizi ya kumsikiliza Sankuu kijijni kwetu - vikundi vya ngoma, band za wanafunzi, kwata, magawaride nk.

Ilifika siku ya ya Sankuu kusema alichowaitia wananchi mbele ya Rais. Sankuu alikuwa haongei kiswahili ni mwendo wa kiingereza mwanzo mwisho - kitendo hicho kiligrab attention za watu na kusababisha Rais badala ya kumsikiliza akageuka kuwa mkalimani! Rais alibabaika kukalimani, hadi akawa akisubiri Sankuu aongee na kutafsiri kijumlajumla.

Msomi Sankuu aliwahutubia wananchi kupitia ukalimani wa Baba wa Taifa. Alijitambulisha kama msomi wa sayansi ya mambo ya anga kutoka Urusi. Huko amehitimu masomo ya juu zaidi na kuajiriwa kufanya kazi katika viwanda vya kutengeneza ndege na rocket. Kwamba ameongea na serikali ya Urusi na wamekubali kumpa ndege mbili kwa ajili ya Tanzania na meli 2 ambazo zitaanza safari ya kuja nchini iwapo Rais angeridhia. Wananchi pamoja na Rais walisisimkwa sana na ahadi za Sankuu.

Lakini kuna jambo moja alimaliza nalo. Akasema pamoja na kwamba mimi naleta ndege na meli ambazo zitakuwa mali ya Taifa, nimeahidiwa mabasi matatu kwa ajili ya kijiji. Lakini sitakubali yaje bila kuwa na barabara zinazoeleweka. Rais aliahidi ndani ya muda sifuri kwenda kushughulikia bajeti ya kujenga barabara kijijini kwetu mpaka makao makuu ya mkoa ambayo ilikuwa ni mjini.

Hadi hivi sasa ninapomaliza kuandika, barabara za kijijini kwetu ni lami ambayo ipo tangu miaka ya 1970.

Sankuu baada ya hotuba yake na ziara ya Rais, aliahidi kuwa kuanzia kesho yake ataanza mchakato wa kufuatilia Meli, ndege na Mabasi, lakini mchakato huo angeufanya akiwa Moscow, hivyo hakuonekana tena mpaka hivi sasa.

Naamini Nyerere ilikuwa akikumbuka kitendo cha Sankuu alicheka mwenyewe mpaka hadi kupaliwa.

Sankuu ndio mtu pekee tu ambaye kila nikimtafakari huwa simumalizi.
1
1 Image
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5211
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#2

Interesting story @RealityKing
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
RealityKing
Senior Expert Member
Reactions: 26
Posts: 163
Joined: 7 years ago
Has thanked: 10 times
Been thanked: 14 times

#3

Eli wrote: 6 years ago Interesting story @RealityKing


Naona sasa kuna mention feature, itapendeza sasa @Eli !
0
User avatar
Forbidden_Technology
Senior Expert Member
Reactions: 16
Posts: 113
Joined: 9 years ago
Has thanked: 25 times
Been thanked: 14 times

#4

Dr. Shika na Sankuu ni kiboko, forum na mambo mapya, itapendeza sasa! @Eli @RealityKing
0
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5211
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#5

Dr. Shika sio wa mchezo, viewtopic.php?f=196&t=5598&sid=e7ca9737 ... 2991bfa3c0


@Simulink

@RealityKing Story ya Shika umeiachia njiani, iendeleze bado kuna mengi, anazidi kutoa episodes.

Critical Thinkers, sasa hivi unaweza kukopi na kupaste au kuandika tu web address fulani, then info kutoka website husika zitakuwa pulled na dislayed magically: Kwa mfano, jaribu kuandika websites za Google, Facebook, Twitter:

www.google.com

www.facebook.com

www.twitter.com

Inapendeza sasa.
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
Post Reply

Return to “Story Writing, Fiction and Nonfiction”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 1 guest