• Active Topics 

Baadhi ya Shule Tanzania Hutoza Ada na Michango kati ya Milioni 60 na Milioni 100

Are you satisfied with the current education situation in Africa countries? Do you think there should be reforms in Africa education systems, why?
Post Reply
User avatar
Eli
Senior Expert Member
Reactions: 183
Posts: 5212
Joined: 9 years ago
Location: Tanzania
Has thanked: 75 times
Been thanked: 88 times
Contact:

#1

Wakati Serikali ikihaha kuandaa mwongozo kwa vyuo na shule binafsi za msingi na sekondari ili kudhibiti viwango vya ada, hali ni tofauti kwenye shule za kimataifa ambazo zinaonekana kama zinachuana kwa kuwa na ada kubwa.

Wakati ada ya juu kwa shule zinazotumia Kiingereza kuanzia elimu ya msingi ni kati ya Sh 2 milioni na Sh 3 milioni, ada ya shule za kimataifa zilizopo nchini inafikia hadi Sh 60 milioni kwa mwaka, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwenye shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa.

Uchunguzi huo unaonyesha kuwa mwanafunzi wa chekechea hutakiwa kulipa hadi Sh 35 milioni kwa mwaka na fedha hizo hulipwa kwa kutumia dola za Kimarekani.

Baadhi ya shule zinapokea wanafunzi wenye asili ya Asia, nyingine hupokea wanafunzi kutoka nchi tofauti bila ya kubagua na ni dhahiri kuwa hata wazazi wa watoto ni wale wa kipato kikubwa.

Shule nyingi zinatumia Kiingereza katika kufundisha masomo yote darasani kwa mitaala ya kimataifa na walimu wa kigeni ambao wanalipwa mishahara kwa viwango vya kimataifa.

Wanafunzi wanaosoma katika shule hizo wanaishi mazingira tofauti na wanaosoma katika shule za kawaida. Mwananchi lilishuhudia baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa wamevaa kaptula, bukta na sketi zinazoacha wazi mapaja, kufuga rasta huku wavulana wakiwa huru kufuga nywele, na kuvaa hereni bila kubanwa na sheria.
 
Ada na Michango ya Shule

Kwa kuzingatia nyaraka za kujiunga na shule ya International School of Tanganyika (IST) (Shule nyingine inayofanana na IST ni International School of Moshi) iliyoko Masaki, ada ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wa chekechea ni Sh 35.9 milioni; darasa la tatu hadi la tano ada ni Sh 39.8 milioni na kwa wale wanaoingia darasa la sita, la saba na la nane ni Sh 46. 3 milioni huku darasa la tisa na la kumi ada ni Sh 49.2 milioni.

Mchanganuo wa ada kwa mwanafunzi anayeingia darasa la 11 na 12 ni Sh 59.4 milioni. Mbali ya ada hiyo, mwanafunzi hutakiwa pia kulipiwa gharama za ujenzi, ada ya dharura, fomu ya kujiunga shuleni pamoja na michango mingine ambavyo jumla ni Sh 19.8 milioni.

Shule nyingine ambayo tozo zake - ada na michango mingine – imefuata mkondo huo ni Braeburn iliyoko barabara ya Bagamoyo, Africana. Ada ya mwanafunzi wa chekechea ni Sh 12.7 milioni kwa mwaka.

Mwaka wa kwanza na wa pili ambao ni sawa na darasa la kwanza na la pili hulipa Sh 19.3 milioni. Darasa la tatu hadi la sita Sh 21.1 milioni na darasa la saba hadi la tisa (sekondari) ni Sh 25.4 milioni. Mwanafunzi anayejiunga na shule ya msingi ya Readers Rabbit iliyoko Masaki hutakiwa kulipa kiasi cha Sh 24.1 milioni kwa mwaka.

Soma zaidi hapa: Shule Dar yatoza Sh 60 milioni
0
TSSFL -- A Creative Journey Towards Infinite Possibilities!
Post Reply

Return to “Africa Education Sytems”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 2 guests