• Active Topics 

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye Afukuzwa Uwaziri

Post Reply
XtremeNews
Reactions:

#1

Siku moja baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye kupokea taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza kile kilichodaiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds TV akiwa na askari wenye bunduki kwa nia ya kushinikiza habari ya kashfa iliyomhusu Askofu Gwajima kurushwa, Nape alienguliwa nafasi ya uwaziri.





Kuenguliwa kwa Waziri Nape kulifutia baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kupelekea nafasi ya Nape kuchukuliwa na Dr. Harrison George Mwakyembe. Kitendo cha Nape Moses Nnauye kufukuzwa uwaziri kinahusishwa moja kwa moja na dhamira yake na nia yake ya kuunda tume ya kuchunguza kilichotokea kutokana na habari zilizotapakaa kuhusu mkuu wa mkoa kuvamia katika studio za Clouds TV, huku akiahidi kufikisha uchunguzi huo ngazi za juu kwa hatua zaidi, ikiwemo ofisi ya Rais.



Image

Nape Nnauye alikumbana na kashikashi kadhaa Machi 23, 2017, ikiwemo madai ya kutishiwa bastola na mtu anayedaiwa kuwa ni askari kanzu, wakati alipotaka kuongea na waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya uongozi katika wizara aliyokuwa akiiongoza.








Habari zaidi:

- http://www.msn.com/en-za/news/world/tan ... spartanntp

- http://www.bbc.com/news/live/world-africa-39261557

- http://www.dailymail.co.uk/wires/afp/ar ... usion.html

Updates:

Nape Nnauye ametweet video ya wimbo uliobeba maudhui "Haki huinua taifa", ambamo moja ya waimbaji katika video hiyo ni Rais John Pombe Magufuli:

Attachments
JPM_sacks_Nape.jpg
(64 KiB) Not downloaded yet
JPM_sacks_Nape.jpg
(64 KiB) Not downloaded yet
Post Reply

Return to “World News & Politics”

  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 0 guests